TAARIFA YA KIKAO CHA KWANZA CHA TAASISI YA MUUNGANO DEVELOPMENT COMMUNITY SERVICES (MDCS) KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO CHARIS FOOD PLUS TAREHE 19.02.2017 SAA 09:00 ASUBUHI.
WALIOHUDHURIA KIKAO.
WADHIFA WAO
1.      NduguChikumbiroBwire
Mwenyekitiwa Muda
2.      Ndugu Omary Mbaraka
Katibuwamuda
3.      Ndugu Daniel Ngutu
Mjumbe
4.      Ndugu Joseph Bwire
Mjumbe
5.      BiPaskazia Alex
Mjumbe
6.      Bi Sophia John
Mjumbe
WASIOHUDHURIA KIKAO
WADHFA WAO
1.      Salah Mtegule
Mjumbebilataarifa
2.      MirumbeChacha
Mjumbebilataarifa
3.      Kazungu Adam
Mjumbebilataarifa
4.      Swaumu Omari
Mjumbebilataarifa
5.      Witness Mugeta
Mjumbebilataarifa
6.      OnesmoMoyo
Mjumbebilataarifa
7.      Esseko
Mjumbebilataarifa
8.      SalumPossa
Mjumbebilataarifa
9.      Joseph Nyamuhanga
Mjumbebilataarifa
10.  John Mark Magesa
Mjumbebilataarifa
11.  Elidaimakasambala
Mjumbebilataarifa
WALIOOMBA RADHI
WADHFA WAO
1.      PaguSingili
MjumbeAlikuaKazini
2.      RamsonMasale
MjumbeAlikuaKazini
3.      Deus Alex
MjumbeAlikuaKazini
4.      AbubakariMtani
MjumbeAlikuamsibanikigamboni DSM
5.      Merian Joseph
MjumbeAlikuaKazini
6.      Omary Kombo
MjumbeAlikuaKazini
7.      Sankey Kajange
MjumbeAlikuaKazini
8.      MkuliChacha
MjumbeAlikuaKazini
9.      Samuel Mlaga
Mjumbealikuanadharurachuoni
10.  Adam Mwasa
MjumbeAlikuaKazini

KUFUNGUA KIKAO

Kikao kilifunguliwa mnamosaa 09:00 asubuhi, na mwenyekiti wa muda wa (MDCS) Alianza kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria.Pia aliwaomba washiriki kutoa mchango wao wa mawazo kwa agenda zilizoletwa mbele ya kikao.

AGENDA YA KIKAO: 1/1 KUCHAGUA VIONGOZI WA TAASISI

Hapa agenda hii ilikumbana na changamoto ya mahudhurio ya wajumbe kua wachache hivyo basi mjumbe mmoja alipendekeza uchaguzi huu wa viongozi ufanyike kikao kijacho tutakapokua na wajumbe wakutosha. Kwahio kwa pamoja tulikubaliana na hilo.

 AGENDA YA PLILI: 2/1 KUCHAGUA JINA LA UMOJA/TAASISI

Hapa wajumbe wawili walipendekeza majina yafuatayo, mjumbe wa kwanza alipendekeza jina liwe mshkamano na mjumbe wa pili alipendekeza jina liwe muungano, Majina haya yalipitishwa na baada ya hapo tukachagua jina la muungano kua ndio bora Zaidi hapo ndipo mjumbe wa tatu alimalizia jina hilo na kua “Muungano Development Community Services” yaani (MDCS) Ili kuleta maana Zaidi kutokana na mambo ambayo tutajihusisha nayo. Wote tulikubaliana jina liwe hilo.

AGENDA YA TATU: 3/1 KIINGILIO NA ADA KWA WANA TAASISI.

Kiingilio.

Kwa upande wa kiingilio wajumbe mbalimbali walitoa mapendekezo yao katika hili, ikumbukwe kua Kiingilio hutolewa maramoja pale tu mjumbe anapojiunga na MDCS. Mapendekezo yalikua hivi, Kiingilio kiwe, mjumbe wa kwanza alipendekeza iwe shilingi 20,000/= mwinginge alipendekeza 25,000/= mwingine 30,000/=na wa mwisho50,000/=

Ada.

Hapa wajumbe pia walipendekeza ada ambayo itachangiwa na kila mjumbe ifikapo mwisho wa mwezi kama ifuatavyo, mjumbe wa kwanza alipendekeza ada iwe shilingi 40,000/= mwingine 15,000/= mwingine 20,000/= na wa mwisho akapendekeza iwe shilingi 10,000/=

Kwa pamoja tulikubaliana tuje tuamue kikao kijacho juu ya kiingilio na Ada halisi kwa wajumbe.

AGENDA YA NNE: 4/1 NANI ANASTAHILI KUSAIDIWA KATIKA TAASISI YETU


Hapa wajumbe tulipanga makundi matatu ambayo tulilenga Zaidi katika upande waMaafa, Sherehe na Kuhudumia Jamii Kwa pamoja tulikubaliana  kama ifuatavyo hapa chini tukichambua moja baada ya nyingine katika hizo tatu zilizotajwa hapo juu ambazo ni Maafa,Sherehe na Huduma kwaJamii.

Maafa:

Hapa tulikubaliana kua kuwe na mashart yafuatayo ili mtu aweze kusaidiwa ambayoni:-

Ø Awe mwanachama hai

Ø Mwanachama mwenye familia yake (mke/mume na watoto)

Ø Wazazi wa mwanachama hapa tumelenga (baba na mama mzazi) wa mwanachama.

Ø Wazazi wa pande mbili wa familia ya mwanachama (mama mkwe na baba mkwe.)

Ø Watu tegemezi wanaoishi na mwanachama kama house girl, shamba boy  au Ndugu wa karibu.

Zingatia:

Utapewa msaada huo baada ya kuleta vithibitisho kutoka sehemu husika kulikotokea hayo maafa kama ni msiba au tatizo lingine tupate barua maalum kutoka kwa ofisi ya serikali ya mtaa ambayo inatambua kutokea kwa janga hilo pamoja na namba za mwenyekiti wa serikali ya mtaa ili kujiridhisha Zaidi.

Sherehe:
Kuoa/kuolewa
Hapa tulikubaliana kua kwa mwanachama muoaji/muolewaji atapewa fungu la pesa kiasi maalum lakini taasisi ya MDCS haitahusika na kamati ya sherehe hii ya harusi kwa muoaji/muolewaji ambaye ni mwanachama.

Sherehezingine
Pia kwa sherehe zingine kama vile Hakika/40 Ya mtoto, Kujifungua kwa mwanachama,Kipaimala/wakfu pamoja na Ubatizo. Kwa sherehe hizi taasisi itatoa Kiasi kisichomaalum cha pesa kumpa mwanachama kama hongera.
KuhudumiaJamii.

MDCS  Itasaidia makundi maalum ndani na n je ya serikali. MDCS Itatembelea maeneo mbalimbali ya makundi maalum kama vile Vituo vya kulelea Watoto yatima, Mahakama ya watoto, Walemavu pamoja na wagonjwa mahospitalini.

Hapa pia kulikua na nyongeza kuhusu idadi ya wanachama ambayo tulikubaliana kuwe na idadi maalum ya wanachama na kwa pamoja lengo letu tukakubaliana tuwe na wanachama hamsini (50.)Tutatengeneza Fomu maalum ya kujiunga uanachama. Hii ni baada ya kukubaliana kwa kiingilio na ada ya mwanachama kwa kila mwezi.
AGENDA YA TANO: 5/1 KUFUNGUA AKAUTI YA TAASISI MDCS.
Hapa tulijadili kuhusu namna ya kutunza pesa zetu kama kikundi, hivyo tukakubaliana kuanzisha akauti maalum ya kikundi katika benki ambayo itakua na manufaa kwetu kama vile kukopeshwa pesa,hisa na huduma zingine zenye tija kwa taasisi. Ndipo zikapitishwa benki mbili ambazo ni NMB Bank na Tanzania Posta Bank TPB zitafanyiwa utafiti na wajumbe Itakayokidhi vigezo itafunguliwa hio, Jibu kamili litapatikana kikao kijacho.
Mengineyo.
Kikao kilikua namengineyo na hapa mjumbe aliuliza swali kuhusu endapo mjumbe ataachishwa kazi itakuwaje michangoyake?Mjumbe mmoja alijibu kama Ifuatavyo :

mjumbe ambaye atachangia mfululizo kwa kipindi kisichopungua miezi nane au mwaka Endapo atatoa taarifa taasisi itafikilia kumpa mkopo na ili aendeshe maisha yake na kuendelea kutoa michango ya taasisi.

Au atapewa mda wa kutafuta kazi kwa mda wa miezi miwili atakapopata kazi atalipa miezi ambayo anadaiwa.

MWISHO WA KIKAO.
Mwenyekiti wa muda alifunga kikao kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria kwa kutoa mchango wao wa mawazo,na pia kwa uvumilivu wao.kikao kilifungwa mnamo saa 11:00 asubuhi.
MWENYEKITI….……………………….…………KATIBU………..….…………………..……TAREHE……….……………

UMETHIBITISHWA NA KIKAO

Muhtasari huu Umeandaliwa na kuandikwa na omary mbaraka Katibu wa muda
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

1 comments:

 
Top