TAARIFA YA KIKAO CHA TATU CHA TAASISI YA MUUNGANO DEVELOPMENT COMMUNITY SERVICES (MDCS) KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO CHARIS FOOD PLUS TAREHE 12.03.2017 SAA 02:00 MCHANA.
WALIOHUDHURIA KIKAO.
WADHIFA WAO
1.      Ndugu Chikumbiro Bwire
Mwenyekiti wa Muda
2.      Ndugu Omary Mbaraka
Katibu wa muda
3.      Ndugu David Ngutu
Mjumbe
4.      Bi Paskazia Alex Mauna
Mhadhini wa muda
5.      Ndugu Omary Kombo
Mjumbe
6.      Ndugu Bahame Mizingo
Mjumbe
WASIOHUDHURIA KIKAO
WADHFA WAO
1.      Bi Salah Mtegule
Mjumbe bila taarifa
2.      Ndugu Mirumbe Chacha
Mjumbe bila taarifa
3.      Ndugu Kazungu Adam
Mjumbe bila taarifa
4.      Bi Swaumu Omari
Mjumbe bila taarifa
5.      Bi Witness Mugeta
Mjumbe bila taarifa
6.      Ndugu Onesmo Moyo
Mjumbe bila taarifa
7.      Ndugu Esseko
Mjumbe bila taarifa
8.      Ndugu John Magesa
Mjumbe bila taarifa
9.      Bi Merian Joseph
Mjumbe bila taarifa
10.  Ndugu Elidaima kasambala
Mjumbe bila taarifa
11.  Ndugu Adam Mwasa
Mjumbe bila taarifa
12.  Ndugu Mkuli Chacha
Mjumbe bila taarifa
13.  Ndugu Samuel Mlaga
Mjumbe bila taarifa
14.  Ndugu Bundala Patrick
Mjumbe bila taarifa
15.  Ndugu Abubakari Mtani
Mjumbe bila taarifa
16.  Ndugu Elia ghambuna
Mjumbe bila taarifa
WALIOOMBA RADHI
WADHFA WAO
1.      Ndugu Sankey Kajange
Mjumbe Alikua Kazini
2.      Bi Sophia John
Mjumbe Alikua Udhuru nyumbani kwake
3.      Ndugu Deus Alex
Mjumbe Alikua Kazini
4.      Ndugu Salum Possa
Mjumbe Alikua Kazini
5.      Ndugu Abdul Shabani
Mjumbe Alikua Zanzibar
6.      Ndugu Pagu Singili
Mjumbe Alikua Kazini
7.      Ndugu Joseph Bwire
Mjumbe Alikua Anaumwa
8.      Ndugu Joseph Nyamhanga
Mjumbe Alikua Nje ya jiji la Dar es salaam
9.      Ndugu Mwaja Jcob
Mjumbe Alikua Kazini
10.  Ndugu Ramson Masale
Mjumbe Alikua Kazini
KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa mnamo saa 02:00 Mchana, na mwenyekiti wa muda wa (MDCS) Alianza kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria.Pia aliwaomba washiriki kutoa mchango wao wa mawazo kwa agenda zilizoletwa mbele ya kikao.

KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHOPITA
Baada ya kufungua kikao,katibu wa muda alisoma muhtasari wa kikao kilichopita.Baada ya hapo mwenyekiti wa muda aliwauliza wajumbe kama yaliosomwa na katibu ni sawa na tulivyojadili katika kikao kilichopita, Kwa pamoja wajumbe walisema sawa.

YATOKANAYO.
Katika kikao hiki mjumbe mmoja aliuliza kua ni matatizo yapi yanayopaswa mwana umoja kusaidiwa? Au ni kwa tatizo lolote? Mjumbe mmoja alimjibu kua swala hili tushalijadili katika kikao cha kwanza hivyo ndugu mjumbe unaombwa kurejea katika muhtasari wa kikao cha kwanza kilichopita ili kusoma na kufahamu Zaidi juu ya hilo.

ü  AGENDA YA KWANZA:  1/3 KUCHAMBUA RASIMU YA KATIBA  YA TAASISI

Katiba ndio msingi wa kila kitu katika umoja huu hivyo ni vizuri kuchambua kwa umakini rasimu ya katiba iliyoletwa mbele ya kikao hiki ili tupate katiba rasmi kwa ajili ya umoja wetu. Hapa tulijadili vipengele ambavyo vitakuwepo katika katiba kama ifuatavyo:

Ofisi  - Katiba hapa itaonyesha mahali ilipo ofisi ya umoja wetu, hapa kila mjumbe alipendekeza ofisi iwe wapi, ofisi kuu itakua katika Mkoa wa Dar es salaam ambayo ndo makao makuu ya umoja huu wa MDCS.
kwa upande wa wilaya ndipo mjumbe wa kwanza akasema iwe katika wilaya ya temeke pembezoni ili kukwepa ghalama za kulipia pango endapo ofisi itakua katikati ya jiji.Mjumbe mwingine alipendekeza iwe ilala pembezoni na wa mwisho alipendekeza iwe popote pale ili mladi kusiwe na ghalama kubwa za pango kwakua umoja ndo unaanza na tusijali umbali wa ofisi kwani vikao vitakua na sehemu yake na ofisi itakua sehemu nyingine. Baada ya hapo

mwenyekiti wa muda alimtafuta mwanasheria kwa njia ya simu ili kumuuliza juu ya swala hili kua ni wapi panastahili kuwa ofisi ya umoja wetu kwa bahati mbaya mwanasheria hakupatikana hivyo mada hii tutapata jibu rasmi kikao kijacho ila haitakua na majadiliano tena, kwa pamoja tulikubaliana hivyo.

ü  SIMU YA OFISI  1.1/3  (NAMBA ZA SIMU)
Hapa Katika katiba yetu ni lazima iwe na kipengele kinachoonyesha simu za ofisi na ni vizuri tukiwa na simu ya mezani, lakini kwa vile bado hatuna ofisi tumekubaliana kuwa kwasasa zitumike namba za katibu,mwenyekiti na mweka hadhina kua kama ni namba za ofisi kwa hio kuanzia leo kwa shida yoyote ya kiofisi ni lazima uwasiliane na watu hao na namba zao nia kama ifuatavyo, Katibu, simu namba 0654 29 19 32 Ndugu Omary mbaraka, Mwenyekiti simu namba 0766 93 07 04 Ndugu Chikumbiro Bwire, Na mhadhini Simu namba 0717 33 02 12 Bi. Paskazia Alex Mauna. 

ü  SANDUKU LA POSTA:  1.2/3 (S.L.P/P.O.BOX).
Sanduku la posta hili hutumika kupokea barua zinazotoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi hivyo katika katiba ni lazima kipengele hiki kiwepo, namna ya kufungua na ghalama zake mjumbe mmoja alitolea ufafanuzi kua kuna tofauti ya haya masanduku ya posta ambayo yapo ya binafsi na ya kampuni au taasisi hivyo mjumbe huyu alipewa jukumu hili la kufuatilia na kuleta majibu katika kikao kijacho pia hapa hakuta kua na majadiliano tena ni majibu tu na kuendelea na kikao kwahio tulikubaliana hivyo .

Barua Pepe (E-mail) Hapa pia lazima katiba ionyeshe barua pepe ya umoja huu na ni lazima tuwe na barua pepe, hii itasaidia na itatumika na watu mbalimbali kutuma maoni au ushauri na kuuliza chochote kupitia mtandao, Pia katiba itataja tovuti (Website) ya umoja wetu wa  MDCS

Mjumbe mmoja mwenye ujuzi na haya mambo alielezea kua kwa upande wa Parua pep (E-mail) Zipo za aina mbili, kuna za bure na zakulipia, Barua pepe za kulipia zinaendana na jina la tovuti mfano info@mdcs.org hiyo inalipiwa kwa mwaka shilingi elfu hamsini 50,000/= hadi Elfu sitini na tano 65,000/=, Lakini zipo Barua pepe za bure ambazo haziendani na jina la tovuti, mfano mdcs@gmail.com Kwa upande wa barua pepe tumekubaliana tututmie ya bure.

Tovuti pia zipo za bei nafuu ambazo unalipia Domain name peke yake kwa mwaka ni shilingi elfu therathini 30,000/= kwa domain ya .com  ila pamoja na utengenezaji ni Shilingi elfu hamsini. 50,000/= tovuti itakua na jina la umoja yaani www.mdcs.org  kwa domain ya .org kwa mwaka ni shilingi 35,000/=kwasasa.
Kwa upande wa tovuti ya kulipia zinaghalimu shilingi laki na hamsini kwa mwaka na kuendelea.
Hapa kuna ghalama za Web Hosting,Domain Name Pamoja na Bussiness E-mail huduma zote tatu kwa pamoja ndo zinaghalimu kiasi kisichopungua shilingi laki moja na hamsini na kuendelea

Tulikubaliana itakapofikia kufungua tovuti tutatengeneza ya bei nafuu.

ü  NEMBO YA UMOJA 1.3/3 (LOGO)
Katiba yetu pia itakuwepo na nembo katika kava la nje na nyaraka mbalimbali za umoja huu, na ikumbukwe kua nembo ndio utamburisho wa umoja au kampuni yoyote na tumekubaliana katika nembo yetu kuwe na picha za viashiria vya msaada na  usawa wa kijinsia,zitatengenezwa nembo tatu  zita printiwa na kuletwa mbele ya kikao ili kupendekeza ni ipi inafaa ili tuitumie.
Mengineyo.

 Kikao kilikua na mengineyo na hapa mjumbe allipendekeza kuwepo na kopi ya rasimu ya katiba kwa kila mjumbe ili iwe rahisi wakati wa kujadili ili tumalize kwa haraka Zaidi. Kwa pamoja tulikubaliana na hilo na zoezi litaanza baada ya kikao na karatasi hizo za rasimu zinaanza kwa Ndugu David Ngutu, rasimu ya katiba inayopendekezwa ina kurasa 49 hivyo utaghalamia kutoa kopi kabla ya kikao uwe tayari ushapata kopi.

Pia mjumbe mmoja alitoa wazo kuwa ingekua vizuri Zaidi kama wajumbe watachangia kupitia mitandao ya simu kwa kutuma meseji baada ya kuipitia rasimu ya katiba na kupendekeza wapi parekebishwe hasa kwa wale wasiohudhuria vikao ingependeza Zaidi tupate mawazo yao kwa njia hiyo, Pia tulipitisha kwa hilo atakayeweza kufanya hivyo afanye.


MWISHO WA KIKAO.
Mwenyekiti wa muda alifunga kikao kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria kwa kutoa mchango wao wa mawazo,na pia kwa uvumilivu wao,na kuwataka wakayafanyie kazi yaliozungumzwa na Zaidi aliwaomba wajumbe watoe kopi ya rasimu ya katiba inayopekezwa ili iwe rahisi kwa kikao kijacho kujadili na kupitisha kwa pamoja vipengele tutakavyoona vinafaa katika katiba yetu mpya. Kikao kilifungwa mnamo saa 04:10 Jioni.

MWENYEKITI….……………………KATIBU….………………TAREHE……….……………..…

UMETHIBITISHWA NA KIKAO

1 comments:

 
Top