Kupitia katiba ya MDCS Tanzania kama inavyosema katika sura ya saba ukurasa wa 14 kipengere cha SHEREHE/SENDOFF kinasema hivi;
Mwanaumoja ata kuwa na haki ya kuchangiwa fedha katika sherehe ya arusi na send off kama ndugu pale tu anapooa ,kuolewa,kuoza mtoto wake kama ifuatavyo:
Kila mwanaumoja atachanga Tsh--------------------------
Hivyo basi kupitia kipengele hicho MDCS Imempa mkono wa hongera ndugu Omary Mbaraka kwa kufunga ndoa. Isome hapa chini barua waliomuandikia ambayo ilisainiwa na wajumbe waliomkabidhi.
MBONDOLE KATA YA MSONGOLA,
ILALA MKOA WA DAR ES SALAAM
P.O.BOX 61376 DAR ES SALAAM
TAREHE: 22/10/2017
YAH: KUTOA MKONO WA HONGERA KWA MJUMBE NDUGU OMARY MBARAKA KWA KUFUNGA NDOA
Ndugu! husika na kichwa cha habari hapo juu, Taasisi ya MDCS Kupitia katiba yake kama inavyoeleza katika kipengele cha sherehe kua Tutamchangia mtu yeyote ambae ni mwana MDCS anapotaka kufunga ndoa/kuoa au kuolewa,kipaimara na sherehe zingine zilizotajwa na katiba ya MDCS.
Siku ya tarehe 15/08/2017 Kamati tendaji iliridhia kuchanga kiasi cha shilingi elfu tano kwa kila mwana MDCS Kumchangia Ndugu Omary Mbaraka ambaye anatarajia kufunga ndoa siku ya tarehe 28/10/2017 Jumamosi huko Nyumbani kwao manzese mkoa wa Dar es salaam
Hivyo basi leo Tarehe 27/10/2017 MDCS Inamkabidhi kiasi cha shilingi Elfu hamsini na tano za tanzania 55,000/=bila senti Kama mkono wa hongera ikiwa ni michango ya wanachama wote kumi na moja kila mwanachama amechanga shilingi elfu tano za Tanzania 5,000/=bila senti.
Pesa hizo zilikabidhiwa na ndugu Mjumbe Bahame Mizingo na Mweka hadhina wa muda Baraka Juliasi. Sahihi ya mkabidhi fedha………………..…… Pia zilipokelewa na Ndugu Omary Mbaraka sahihi………………
Imethibitishwa na mwenyekiti wa Taasisi ya Muungano Development Community Service (MDCS) Ndugu CHIKUMBIRO BWIRE Leo Tarehe………../………..…./…….……………Sahihi…………
Kwa matumizi ya ofisi tu.
Maoni ya
Mwenyekiti…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……Jina:……………………….….Sahihi…………………..Tarehe:…………../……………./….........
“(MDCS) Inakutakia kila la kheri katika maisha yako ya ndoa”
0 comments:
Post a Comment