Picha za kuuaga mwili wa mwanachama mwenzetu wa MDCS Ndugu David Nguttu alifariki dunia baada ya kupata ajali ya gari katika mataa ya TAZARA Jijini Dar es salaam siku tarehe 22 mwezi wa 11 mwaka 2017 na kulazwa katika hospitali ya TEMEKE Na kufariki siku ya tar. 26 mwezi wa 11 mwaka 2017
Mbele yake nyuma yetu MDCS Kama kupitia katiba yetu inasema kwa msiba wa mwanachama kila mwanachama atachangia kiasi cha shilingi elfu 20 kama lambilambi kwa familia ya msiba na kwa umoja wetu tulilifanikisha hili na tukapata jumla ya shilingi laki mbili ikiwa ni michango ya wanachama kumi.
Lakini pia wapo marafiki wa MDCS Ambao ni Deusi alex Masatu na Ndugu Puya ambao walichangia kiasi cha shilingi 15,000/= kama rambirambi Deusi alex Alitoa 5000/= na Ndugu PUYA Alitoa shilingi 10,000/= Hivyo jumla ikawa shilingi 215,000/=
Katiba ya MDCS Inasema mtu yeyote atachangiwa ikiwa ni mwanachama hai yaani hana deni la michango yeyote ile hivyo basi kama tungefuata katiba tusinge mchangia ndugu yetu kwasababu alikua na deni hivyo basi tulitoa pesa aliokua anadaiwa kisha kiasi kilichobaki tulikikabidhi kwa familia shilingi 190,000/= tulizikabidhi na marehemu hana deni kwasasa ni mwanachama hai kichama ingawa kimwili hatuko nae.
Kwa pamoja Wana MDCS Tunamuombea mapunziko mema huko aendako mbele yake nyuma yetu .pia tunakaribisha wanachama wapya wanaotaka kujiunga na taasisi yetu ya MDCS TANZNAIA Karibuni sana tufikie malengo tukiwa pamoja.
Kwa pamoja Wana MDCS Tunamuombea mapunziko mema huko aendako mbele yake nyuma yetu .pia tunakaribisha wanachama wapya wanaotaka kujiunga na taasisi yetu ya MDCS TANZNAIA Karibuni sana tufikie malengo tukiwa pamoja.
Picha marehemu hizi hapa wakat anaagwa katika hospitali ya TEMEKE
Jeneza lililokua na mwili wa marehemu David Nguttu Ndege |
Mwenyekiti wa MDCS Ndugu Chikumbiro Bwire alieshikiria Msalaba |
Ndugu jama na marafiki wakiaga mwili wa marehemu |
Mwili wa marehemu ukiingizwa katika gari kwaajili kusafirisha kwenda MUSOMA kwaajili ya maziko |
safari ya kwenda musoma ilianza ndugu jamaa na marafiki wakitawanyika eneo la tukio baada ya kuaga |
0 comments:
Post a Comment