Habari ndugu wanachama wa MDCS napenda kuwapa taarifa ya kikao cha ishirini na moja kilichofanyika katika eneo letu tulilonunua mwaka mmoja uliopita katika kijiji cha Nasako kitongoji cha Mwanadilatu wilaya ya mkulanga mkoani pwani ikipakana na wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es salaam,
Mbali na kikao tulifanikiwa kulifanyia usafi eneo letu kwa kadri tulivyoweza kutokana na uchache wetu tuliohudhuria kikao hicho ukilinganisha na idadi kubwa ya wanachama ambao hawakuhudhuria na wengina hawakutoa hata taarifa za kutokufika kwao.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za wanachama tukiwa tunafanya usafi katika eneo hilo
baada ya kazi tulikuja kunawa hapa na kunywa maji katika kisima cha maji safi kilichopo karibu na eneo letu |
mjumbe kombo akiwa kazini ameshika jembe |
mwenyekiti akiwa upande mwingine akipambana |
Changamoto kubwa ni madeni ya wanachama ambao wamekopa na wamezidisha siku za kulipa hivyo tumeanzimia kufuatilia kwa karibu zaidi kwa wadaiwa wote na pia kuhamasishana juu ya kulipa michango ya ada ya kila mwezi madeni yatasomwa kila kikao kikao kwa wadaiwa na marejesho ya mikopo ikiwezekana iwasilishe siku ya kila kikao au uje na risiti ya kulipia deni lako kama umelipia benki
Pia tuna ukosefu wa watu wawili upande wa signatory hivyo kikao kikaamua kumchagua Mjumbe Linua Wiliam na ERlia Ghambuna kwa ajili ya kujaza nafasi ya hizo mbili ambazo zilikua wazi
Kikao kingine kitakua mwezi ujao eneo ni lile lile kama ilivyopendekezwa na wajumbe walihudhuria kikao kwa ujumla kikao kilikua safi na kila mtu alifurahi
Hivyo basi kwa wewe ambaye hukuhudhuria jitahidi kikao kijachpo uwepo kwani mchango wako ni muhimu sana
Asanteni ni mimi wenu katibu MDCS
Omary Mbaraka
0 comments:
Post a Comment