ifuatayo ni riporti ya kikao cha kumi na 18 kilichofanyika katika ukumbi wa white bar uliopo dar es salaam maeneo ya mtoni mtongani kwa azizi ali
AGENDA ZA KIKAO
Kufungua kikao, Kusoma muhtasari wa kikao kilihopita, Yatokayo, Ripoti ya fedha, Maendeleo ya kikundi, Mengineyo na Kufunga kikao.
Ndugu wanachama hizo ndizo zilikua agenda za kikao chetu lakini mambo muhimu ambayo unapaswa kuyafamu ni kuhusiana YATOKANAYO na kikayo kilichopita ambapo hapa kulikuwa na majibu ya utekelezaji wa yale tuliokubaliana katika kikao cha kumi na saba. na pia RIPOTI YA FEDHA Pamoja na MAENDELEO YA Kikundi,
YATOKANAYO
Hapa kulikua na majibu ya kikao kilichopita cha 17 ambapo tulikubaliana juu ya kutafuta eneo ambalo tutalitumia wenyewe kwaajili ya miradi yetu mbali mbali ikiwemo mradi wa kuku ambao tuliujadili katika kikao cha kumi na 16 ila tuliusitisha kutokana na maoni ya mjumbe mmoja kuwa ni vizuri tukawa na eneo letu kwanza kisha ndio mradi ufuate.
Majibu ni kwamba eneo lilipatikana na kununuliwa, eneo hili lipo mkoa wa pwani wiliya ya mkulanga kijiji cha nasako kitongoji cha mwanadilatu eneo hili linakana na wiliya ya ilala mkoa wa dar es salaam ukitaka kufika unatakiwa kupanda magari yanayoelekea Mvuti kisha shuka kituo kinachoitwa KITONGA Halafu utapanda pikipiki mpaka eneo husika ni 1500 au unaweza kutembea kwa miguu. tumenunua eneo lenye ukubwa wa futi 40 kwa 103 kwa ghalama ya shilingi milioni moja laki tatu na elfu ishirini pamoja na kodi ya serikali ya asimia kumi wakati eneo halisi bei yake ni 120000/= kila futi 20 kwa 40 ni laki 6.
Majibu ya computer, mrejesho mwingine ni ununuzi wa kompyuta kama tulivyokubaliana katika kikao cha 17 ukweli ni kwamba kompyuta ilinunuliwa kwa ghalama ya shilingi laki mbili na themanini 2800000/= printer 100,000/= na lim paper 10,000/= hivyo kwasasa mali za kikundi ni kiwanja chenye ukubwa wa futi 40 kwa 103, Compyuter, na printer.
aina ya computer tulionunua ni HP yenye Hard disk 320, process core 2 duo na RAM 2GB |
printer yenye uwezo wa kuprint brack na collored, kupy black na colloured,na ku scan document |
Swala la katiba
baada ya kununuliwa computer lengo moja wapo lilikua kupangilia katiba yetu katika mpangilio maalum tuliopewa na afisa maendeleo ya jamii katika ofisi ya mtendaji kata wa msongola mtaa wa mbondole ambako ndiko tulikoanzia harakati za usajili wa katiba yetu, kutokana na ubize wa hapa na pale zoezi hili la kuhariri katiba limekua gumu kwa upande wa katibu lakini ndugu mhadhini alisema atalifanyia kazi na kama atakutana na changamoto yoyote atatwambia.
RIPOTI YA FEDHA
Kuhusian na ripoti mhadhini alisomwa na kuonekana madeni ya wanachama ambao yapo nje ni mengi kuliko kiasi kilicho benki hapo ndipo wajum,be waliohudhuria kikao kuomba wasomwe wadaiwa sugu ambao wanazorotesha maendeleo ya kikundi yaani wamekopa mda mrefu na muda wao wa kurejesha umefika lakini hawajarejesha, hapa mhadhini aliomba muda awape taarifa kwanza, na tutakubaliana kikao kijacho wadaiwa sugu wote watatajwa lakini pia tukakubaliana kwa wanachama wote kwamba mwanachama msumbufu au mdaiwa sugu apunguziwe kiwango cha kukopa, na sheria ya mikopo ifuatwe kikatiba ambapo haruhusiwi mtu kukopa kama ana deni,
MAENDELEO YA KIKUNDI,
Kwa kifupi maendeleo sio mazuri kutokana na watu kutorejesha mikopo kwa wakati pia michango ya kusaidia hairidhishi kwani ndugu bahame amechangiwa na wanachama 18 tu kati ya wanachama 18 waliohai kichama wengine hawajachanga hivyo kwa mujibu wa katiba hawana sifa ya kukopa wala kuchangiwa mpaka wachange kwanza,
pia kulikua na taarifa ya huzuni kwa wanachama wawili ambao walifiwa na baba zao wazazi wanatakiwa kuchangiwa shilingi elfu kumi kwa kila mwanachama kwa mujibu wa katiba. wachangishaji wa michango hii ni
Steven Mathias anachangisha msiba wa baba yake mzazi Deus Ngege
Kikoisi Rotoishe anachangisha msiba wa baba mzazi Linusi William
MENGINEYO
Katika kikao hiki kulikua na mengineyo qa hapa mjumbe aliuliza swali kuhusian na ajali aliopata mwanachama mwenzetu ndugu mwakabungu joseph kwanini uongozi ulikaa kimya, majibu yake yalijibiwa na katibu kupitia katiba
“sura ya saba 2.0. iii) AFYA/MISAADA/SHEREHE NA UANA UMOJA ugonjwa: A. Ugonjwa utakaohitaji mwanaumoja kuchangiwa ni lazima kamati tendaji ijirizishe kuwa mwanaumoja huyo anahitaji kuchangiwa na anayechangiwa awe ameruhusiwa na katiba,na endapo itaonekana hitajio hilo lipo: B. Kila mwana umoja atachangia kiwango kilicho pendekezwa na umoja kwa wakati huo”
wajumbe wakaridhika na hilo ila tulikubaliana inapotokea tukio la ghafla kama hilo kiitishwe kikao cha dharula kujadili hilo pia tulichangua wasaidizi wa kamati tendaji wa muda ambao ni Bahame Mizingo Mwenyekiti Msaidizi na Paul Bugoche Katibu Msaidizi Mhadhini atabaki huyo huyo mmoja kwausalama zaidi wa fedha.
Hio ndio taarifa muhimu kuhusian kikao cha kumi 18 kilichofanyika 01 july 2019 hivyo ukiwa kama mwanachama zingatia mambo muhimu yalizungumzwa ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya ada na mkopo kwa wakati na kama ni mdaiwa sugu utatajwa katika kikao kijacho, Mchango wa kuchangia msiba au sherehe ni lazima na ipo kikatiba.Vikao vitakuwa kila mwezi ili kujadili maendeleo ya kikundi na kutekeleza yale ya msingi.
Imeandikwa na kuchapwa na katibu wa kikundi MDCS,
Ndugu: Omary Mbaraka
0 comments:
Post a Comment