TAARIFA YA KIKAO CHA
TATU CHA TAASISI YA MUUNGANO DEVELOPMENT COMMUNITY SERVICES (MDCS)
KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO CHARIS FOOD PLUS TAREHE 12.03.2017 SAA
02:00 MCHANA.
WALIOHUDHURIA KIKAO.
|
WADHIFA WAO
|
1.
Ndugu
Chikumbiro Bwire
|
Mwenyekiti wa Muda
|
2.
Ndugu Omary
Mbaraka
|
Katibu wa muda
|
3.
Ndugu David
Ngutu
|
Mjumbe
|
4.
Bi Paskazia
Alex Mauna
|
Mhadhini wa muda
|
5.
Ndugu Omary
Kombo
|
Mjumbe
|
6.
Ndugu Bahame
Mizingo
|
Mjumbe
|
|
|
WASIOHUDHURIA KIKAO
|
WADHFA WAO
|
1.
Bi Salah
Mtegule
|
Mjumbe bila taarifa
|
2.
Ndugu Mirumbe Chacha
|
Mjumbe bila taarifa
|
3.
Ndugu Kazungu
Adam
|
Mjumbe bila taarifa
|
4.
Bi Swaumu Omari
|
Mjumbe bila taarifa
|
5.
Bi Witness
Mugeta
|
Mjumbe bila taarifa
|
6.
Ndugu Onesmo
Moyo
|
Mjumbe bila taarifa
|
7.
Ndugu Esseko
|
Mjumbe bila taarifa
|
8.
Ndugu John
Magesa
|
Mjumbe bila taarifa
|
9.
Bi Merian
Joseph
|
Mjumbe bila taarifa
|
10.
Ndugu Elidaima
kasambala
|
Mjumbe bila taarifa
|
11.
Ndugu Adam
Mwasa
|
Mjumbe bila taarifa
|
12.
Ndugu Mkuli
Chacha
|
Mjumbe bila taarifa
|
13.
Ndugu Samuel
Mlaga
|
Mjumbe bila taarifa
|
14.
Ndugu Bundala
Patrick
|
Mjumbe bila taarifa
|
15.
Ndugu Abubakari
Mtani
|
Mjumbe bila taarifa
|
16.
Ndugu Elia
ghambuna
|
Mjumbe bila taarifa
|
|
|
WALIOOMBA RADHI
|
WADHFA WAO
|
1.
Ndugu Sankey
Kajange
|
Mjumbe Alikua Kazini
|
2.
Bi Sophia John
|
Mjumbe Alikua Udhuru nyumbani kwake
|
3.
Ndugu Deus Alex
|
Mjumbe Alikua Kazini
|
4.
Ndugu Salum Possa
|
Mjumbe Alikua Kazini
|
5.
Ndugu Abdul
Shabani
|
Mjumbe Alikua Zanzibar
|
6.
Ndugu Pagu
Singili
|
Mjumbe Alikua Kazini
|
7.
Ndugu Joseph
Bwire
|
Mjumbe Alikua Anaumwa
|
8.
Ndugu Joseph
Nyamhanga
|
Mjumbe Alikua Nje ya jiji la Dar es
salaam
|
9.
Ndugu Mwaja
Jcob
|
Mjumbe Alikua Kazini
|
10.
Ndugu Ramson
Masale
|
Mjumbe Alikua Kazini
|
KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa mnamo saa 02:00 Mchana,
na mwenyekiti wa muda wa (MDCS)
Alianza kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria.Pia aliwaomba washiriki
kutoa mchango wao wa mawazo kwa agenda zilizoletwa mbele ya kikao.
KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHOPITA
Baada ya kufungua kikao,katibu wa
muda alisoma muhtasari wa kikao kilichopita.Baada ya hapo mwenyekiti wa muda
aliwauliza wajumbe kama yaliosomwa na katibu ni sawa na tulivyojadili katika kikao
kilichopita, Kwa pamoja wajumbe walisema sawa.
YATOKANAYO.
Katika kikao hiki mjumbe mmoja
aliuliza kua ni matatizo yapi yanayopaswa mwana umoja kusaidiwa? Au ni kwa
tatizo lolote? Mjumbe mmoja alimjibu kua swala hili tushalijadili katika kikao
cha kwanza hivyo ndugu mjumbe unaombwa kurejea katika muhtasari wa kikao cha
kwanza kilichopita ili kusoma na kufahamu Zaidi juu ya hilo.
ü AGENDA YA KWANZA: 1/3 KUCHAMBUA RASIMU YA KATIBA YA TAASISI
Katiba ndio
msingi wa kila kitu katika umoja huu hivyo ni vizuri kuchambua kwa umakini
rasimu ya katiba iliyoletwa mbele ya kikao hiki ili tupate katiba rasmi kwa ajili
ya umoja wetu. Hapa tulijadili vipengele ambavyo vitakuwepo katika katiba kama
ifuatavyo:
Ofisi - Katiba hapa itaonyesha mahali ilipo ofisi
ya umoja wetu, hapa kila mjumbe alipendekeza ofisi iwe wapi, ofisi kuu itakua
katika Mkoa wa Dar es salaam ambayo
ndo makao makuu ya umoja huu wa MDCS.
kwa upande wa
wilaya ndipo mjumbe wa kwanza
akasema iwe katika wilaya ya temeke
pembezoni ili kukwepa ghalama za kulipia pango endapo ofisi itakua katikati ya
jiji.Mjumbe mwingine alipendekeza iwe ilala
pembezoni na wa mwisho alipendekeza iwe popote pale ili mladi kusiwe na ghalama
kubwa za pango kwakua umoja ndo unaanza na tusijali umbali wa ofisi kwani vikao
vitakua na sehemu yake na ofisi itakua sehemu nyingine. Baada ya hapo
mwenyekiti wa
muda alimtafuta mwanasheria kwa njia ya simu ili kumuuliza juu ya swala hili
kua ni wapi panastahili kuwa ofisi ya umoja wetu kwa bahati mbaya mwanasheria
hakupatikana hivyo mada hii tutapata jibu rasmi kikao kijacho ila haitakua na majadiliano
tena, kwa pamoja tulikubaliana hivyo.
ü SIMU YA OFISI 1.1/3 (NAMBA ZA SIMU)
Hapa Katika
katiba yetu ni lazima iwe na kipengele kinachoonyesha simu za ofisi na ni
vizuri tukiwa na simu ya mezani, lakini kwa vile bado hatuna ofisi
tumekubaliana kuwa kwasasa zitumike namba za katibu,mwenyekiti na mweka hadhina
kua kama ni namba za ofisi kwa hio kuanzia leo kwa shida yoyote ya kiofisi ni
lazima uwasiliane na watu hao na namba zao nia kama ifuatavyo, Katibu, simu
namba 0654 29 19 32 Ndugu Omary mbaraka, Mwenyekiti simu namba 0766
93 07 04 Ndugu Chikumbiro Bwire, Na mhadhini Simu namba 0717 33 02 12 Bi. Paskazia Alex Mauna.
ü SANDUKU LA POSTA: 1.2/3 (S.L.P/P.O.BOX).
Sanduku la posta hili hutumika
kupokea barua zinazotoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi hivyo katika
katiba ni lazima kipengele hiki kiwepo, namna ya kufungua na ghalama zake mjumbe
mmoja alitolea ufafanuzi kua kuna tofauti ya haya masanduku ya posta ambayo
yapo ya binafsi na ya kampuni au taasisi hivyo mjumbe huyu alipewa jukumu hili la
kufuatilia na kuleta majibu katika kikao kijacho pia hapa hakuta kua na
majadiliano tena ni majibu tu na kuendelea na kikao kwahio tulikubaliana hivyo .
Barua Pepe (E-mail) Hapa pia lazima katiba ionyeshe barua pepe ya umoja huu na ni lazima
tuwe na barua pepe, hii itasaidia na itatumika na watu mbalimbali kutuma maoni
au ushauri na kuuliza chochote kupitia mtandao, Pia katiba itataja tovuti (Website) ya umoja wetu wa MDCS
Mjumbe mmoja mwenye ujuzi na haya
mambo alielezea kua kwa upande wa Parua pep (E-mail) Zipo za aina mbili, kuna
za bure na zakulipia, Barua pepe za kulipia zinaendana na jina la tovuti mfano info@mdcs.org hiyo inalipiwa kwa mwaka shilingi
elfu hamsini 50,000/= hadi Elfu sitini na tano 65,000/=, Lakini zipo Barua pepe
za bure ambazo haziendani na jina la tovuti, mfano mdcs@gmail.com Kwa upande wa barua pepe
tumekubaliana tututmie ya bure.
Tovuti pia
zipo za bei nafuu ambazo unalipia Domain
name peke yake kwa mwaka ni shilingi elfu therathini 30,000/= kwa domain ya
.com ila pamoja
na utengenezaji ni Shilingi elfu hamsini. 50,000/= tovuti itakua na jina la umoja
yaani www.mdcs.org kwa domain ya .org kwa mwaka ni shilingi 35,000/=kwasasa.
Kwa upande wa tovuti ya kulipia
zinaghalimu shilingi laki na hamsini
kwa mwaka na kuendelea.
Hapa kuna ghalama za Web Hosting,Domain Name Pamoja na Bussiness
E-mail huduma zote tatu kwa pamoja ndo zinaghalimu kiasi kisichopungua
shilingi laki moja na hamsini na kuendelea
Tulikubaliana itakapofikia kufungua
tovuti tutatengeneza ya bei nafuu.
ü NEMBO YA UMOJA 1.3/3 (LOGO)
Katiba yetu pia itakuwepo na nembo
katika kava la nje na nyaraka mbalimbali za umoja huu, na ikumbukwe kua nembo
ndio utamburisho wa umoja au kampuni yoyote na tumekubaliana katika nembo yetu
kuwe na picha za viashiria vya msaada na usawa wa kijinsia,zitatengenezwa nembo tatu zita printiwa na kuletwa mbele ya kikao ili
kupendekeza ni ipi inafaa ili tuitumie.
Mengineyo.
Kikao kilikua na mengineyo na hapa mjumbe
allipendekeza kuwepo na kopi ya rasimu ya katiba kwa kila mjumbe ili iwe rahisi
wakati wa kujadili ili tumalize kwa haraka Zaidi. Kwa pamoja tulikubaliana na
hilo na zoezi litaanza baada ya kikao na karatasi hizo za rasimu zinaanza kwa Ndugu
David Ngutu, rasimu ya katiba inayopendekezwa ina kurasa 49 hivyo utaghalamia
kutoa kopi kabla ya kikao uwe tayari ushapata kopi.
Pia mjumbe
mmoja alitoa wazo kuwa ingekua vizuri Zaidi kama wajumbe watachangia kupitia
mitandao ya simu kwa kutuma meseji baada ya kuipitia rasimu ya katiba na
kupendekeza wapi parekebishwe hasa kwa wale wasiohudhuria vikao ingependeza
Zaidi tupate mawazo yao kwa njia hiyo, Pia tulipitisha kwa hilo atakayeweza
kufanya hivyo afanye.
MWISHO WA KIKAO.
Mwenyekiti wa muda alifunga kikao kwa
kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria kwa kutoa mchango wao wa mawazo,na pia
kwa uvumilivu wao,na kuwataka wakayafanyie kazi yaliozungumzwa na Zaidi
aliwaomba wajumbe watoe kopi ya rasimu ya katiba inayopekezwa ili iwe rahisi
kwa kikao kijacho kujadili na kupitisha kwa pamoja vipengele tutakavyoona
vinafaa katika katiba yetu mpya. Kikao kilifungwa mnamo saa 04:10 Jioni.
MWENYEKITI….……………………KATIBU….………………TAREHE……….……………..…
UMETHIBITISHWA NA KIKAO